Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2021

Furaha Ni Nini?

   Watu wengi hudhani furaha Ni kufanya starehe nyingi au mbalimbali au kuwa na vitu vingi vinavyokupa starehe. Wengine hudhani furaha Ni kuwa na watu Fulani karibu Yako kila Mara,huenda ikawa Ni kweli kwa baadhi ya watu panda wakati mwingine hukufanya ujisikie nafuu kutokana na madhila ya maisha.... Wengine huenda Mbali zaidi na kuwategemea watu kuwa Ni sehemu ya kujipatia furaha... Bila kujua matarajio ya binadamu mwenzio kukupa furaha Ni madogo Sana.     Je furaha Ni Nini Basi!? Furaha Ni amani thabiti kutoka ndani ya moyo wa mtu,ni amani inayoambatana na imani ya kweli na yenye uchanya ndani yake,kuwa na furaha sio kukosekana kwa matatizo au tabu mbalimbali hapana ni kukubaliana na hali fulani ya wakati uliopo huku ukipambana kuibadilisha au kuimarisha iwe salama na bora zaidi.    Furaha ni usalama wa hisia zako unaochangiwa na msukumo wa ndani yako mwenyewe wala hapana yeyote anaweza kutoka nje yako na kuijaza furaha ndani yako, ni lazima uwe mtu mweny...

Uhuru ni nini?

 Uhuru ni fursa ya kutenda mema kila wakati tena kila mara,ni fursa ya kuamua namna ya kuishi kwa uchanya wa maisha kila siku na ni wakati wa kila mara kujituma kwa kila namna ya wema kifikia malengo mema na kuiacha dunia ikiwa sehemu Salama ya kuishi kila mara