Furaha Ni Nini?

   Watu wengi hudhani furaha Ni kufanya starehe nyingi au mbalimbali au kuwa na vitu vingi vinavyokupa starehe. Wengine hudhani furaha Ni kuwa na watu Fulani karibu Yako kila Mara,huenda ikawa Ni kweli kwa baadhi ya watu panda wakati mwingine hukufanya ujisikie nafuu kutokana na madhila ya maisha.... Wengine huenda Mbali zaidi na kuwategemea watu kuwa Ni sehemu ya kujipatia furaha... Bila kujua matarajio ya binadamu mwenzio kukupa furaha Ni madogo Sana.

    Je furaha Ni Nini Basi!? Furaha Ni amani thabiti kutoka ndani ya moyo wa mtu,ni amani inayoambatana na imani ya kweli na yenye uchanya ndani yake,kuwa na furaha sio kukosekana kwa matatizo au tabu mbalimbali hapana ni kukubaliana na hali fulani ya wakati uliopo huku ukipambana kuibadilisha au kuimarisha iwe salama na bora zaidi.

   Furaha ni usalama wa hisia zako unaochangiwa na msukumo wa ndani yako mwenyewe wala hapana yeyote anaweza kutoka nje yako na kuijaza furaha ndani yako, ni lazima uwe mtu mwenye furaha ili uweze kuishiriki furaha yako na wengine… kumbuka kimtokacho mtu ndicho kilichomjaa ndani yake… ukiona mtu ana magomvi na kero kwa watu basi hicho ndicho kilochopo ndani yake na sio kingine.

Kuilinda furaha ni jukumu lako mwenyewe na sio la mtu mwingine,binadamu unalazimika kuofanya dunia sehemu salama ya kuishi kwa viumbe vyote,ni ulazima na sio ombi wala sio hiyari ni unalazimika kujenga misingi imara ya kiulimwengu ili jamii nzima ifaidike na wewe.ni jukumu lako na sio la mwingine.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Bin bin pyramid

Japan vs costa rica

MANUEL DE LA SUPRÉMATIE BLANCHE