Vitu 6 vya kukusaidia kujua kama uliyenaye ni mwanamke sahihi wakuoa.

    Linapokuja suala la kuoa ni muhimu zaidi kuamua sahihi maana ni rahisi sana kila jambo kuwa baya kama tutachukua maamuzi mabaya kuoa mwanamke asiye sahihi kwa sababu zisizo za msingi.Sababu hizi za msingi zitakusaidia kujua kama mwanamke ulonae snsfaa kuoa au mpotezeane....
1:ANAJIVUNIA WEWE.
      Kama anajivunia wewe na kukuzungumzia anapokuwa na marafiki zake,wafanyakazi wenzake huyu ni mwanamke wakuoa.kama anafikiria we we ni mwanamke bora mwanamke yeyote anaweza kuwa nawe hii itakusaidia kuamua.

2:YUPO POA NA MARAFIKI ZAKO
       Marafiki wa mwanaume ni sehemu muhimu sana ya ulimwengu wake,mwanaume yeyote anahitaji mwanamke anayejua kuwa marafiki zake ni muhimu kwake pia.Kama anajihusisha sana kujua marafiki zako wanaendeleaje na kupenda kutoka na wewe na marafiki zako hiki kitakusaidia kujua kama ndiye mwanamke wakuoa.

3:ANA MAISHA YAKE
       Kama anaelewa kuwa sio kila jambo lazima likuhusu wewe na anaelewa kuwa maisha yataenda kama yeye atakuwa na vitu vyake na wewe vyakwako.Anaelewa kwamba anatakiwa kukusaidia wewe kufikia ndoto zako huku nayeye akifikia malengo take, hii itakusaidia kuamua.

4:UNAMKUMBUKA ANAPOKUWA HAYUPO NA WEWE.
     Anapokuwa hayupo na wewe huwezi kujizuia unamkumbuka tu.Haijalishi ni kiasi gani unajitahidi kutokumfikiria huwa anakuja tu kwenye mawazo,anapokuwa hivi basi huyu anaweza kufaa kuoa.

5:MNAJITOLEA KWA AJILI YENU
      Kama mwanamke wako hawezi kujitolea kwa ajili yako na wewe hauwezi kujitolea kwa ajili yake sidhani kama ni vyema kumuoa.Ndoa yoyote ili isimame kutoa sadaka ni lazma.Hivyo kama anajitoa sadaka kwa ajili yako na wewe pia vile vile nadhani unaweza ukaoa.

6:NI SHABIKI YAKO NAMBA MOJA.
       Daima husimama na wewe kwenye hali ngumu na haonekani kukiacha kwenye nyakati ngumu.Anakuamini wewe na ndoto zako hata kama wengine hawaziamini.Hata unapokuwa kwenye nyakati ngumu zaidi na anaendelea kuamini kuwa utavuka dhoruba hilo,nadhani anaweza kufaa kuoa.


Asante na ubarikiwe

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Bin bin pyramid

Japan vs costa rica

MANUEL DE LA SUPRÉMATIE BLANCHE