Adamu
Dhana kwamba Mungu alimuumba Adamu pekee kwenye bustani ya edeni Ina UKAKASI KIDOGO. Kama kweli vitabu vyote vitakatifu vinakiri kuwa Mungu Hana dosari,NI mkamilifu na mkuu,mwenye utimilifu na utukufu Basi sidhani Kama yeye Mungu angeweza kusahau kiasi hicho.
Tuseme haya Mungu alimuumba adamu tu duniani,then what? For what purpose? To do what exactly? Kucheza na nyani? Kurukaruka na kunguru? Kula n'a kulala tu? Kuangalia jua linapotoka n'a kuzama? Je majibu ta haya ni yapi?
Kuna sehemu inasema nendeni,mkazae na mkaongezeke mkaijaze duniani,then adamu angetaga? Usitake kuniambia kuwa Mungu aumbe wanyama wote wawili wawili afu adamu awe peke yake tu,maana Hakuna mahali pameandikwa wanyama waliumbwa madume tu kama adamu.Sasa na miti uimbwe,itoe mbegu,izae matunda na vyote hivyo ni kuongezeka afu Mungu asahau kweli kuhusu adamu? Basi tuwaze kwa sauti vitu Vya muhimu kwa Mungu huenda ikawa sio binadamu ni hiyo miti n'a wanyama Basi ndio maana alimuumba binadamu wa mwisho!! (Dhana ya kumuandalia mwanadamu makazi msiiweke hapa maana Mungu ni mkamilifu angeweza kuumba tu vyote kwa Siku Moja)
Kiuhalisia ni kuwa Hakuna mwanamke Bila ya mwanaume na Hakuna mwanaume Bila ya mwanamke hiyo ndio ukweli,kiasili NI hivyo na hata ukifiria Bila box (biblia) unaupata ukweli na unajieleza wenyewe na hauhitaji ushahidi wowote,Mwanaume na mwanamke wameumbwa na majukumu sawa kila mmoja kwa nafasi yake na pia hivi vyote vimeumbwa kuleta usawa kwenye asili ( Kama vile Hakuna mfupi Kama Hakuna mrefu,na pasingekuwa na mashariki Kama Hakuna magharibi) hivyo hata kwetu Hakuna mmoja Bila mwingine,kuna useme kuwa mwanamke anasitiriwa anapoolewa kwa maana pana ni kuwa ameleta usawa kwenye maisha yake na mumewe.
Mwanaume amepewa upeo waa kuona Mambo kwa mbali n'a kwa haraka zaidi ( ndio maana uume wetu unaweza kusimama popote n'a hata bila kuwa n'a mwanamke,ndio maana unaweza kuamka asubuhi uume imesimama) maana yake NI wewe NI wakwanza kufikiria,wakwanza kutafakari,wakwanza kuongoza njia,wewe NI wakwanza kutatua changamoto zenu,wewe ni wakwanza kuunda n'a kutengeneza mipango,mwenye kurehemu na mtashi.
Mwanamke ameumbwa na misuli imara ya uvumilivu,msingi mtakatifu wa hekima na busara,mwanamke ni mwenye kubuni,mwenye kutafakari Mambo kwa kina,mwenye kutia hekima ndani yake,mwenye kufikiri kwa taratibu sana lakini kwa hekima ya hali ya juu (ndio maana kwenye tendo lazima mwanamke aandaliwe,huwezi kumrukia Kama kuku tu,hata kuku anakimbizwa kidogo,ni lazima apewe muda wakutafakari tendo,kukubali hisia kwa hiyari na kufurahia) hiyo ndio hekima ya mwanamke.
Now mwanamke na mwanaume wanakutana kwenye maamuzi yao wenyewe,NI lazima mwanaume kumshirikisha mwanamke kwenye mipango ili maamuzi yawe sahihi,bila kurudi kwenye misingi hii ya kiafrika zaidi ambapo mwanamke alikuwa ni chombo chema,mlezi wa jamii nzima,mwenye rehema na kupewa nafasi ya maamuzi hatuwezi kulea jamii na kumaliza tatizo la unyanyasaji na vitendo viovu,utakatifu tunaoutaka hatuwezi kuupata Kama hatuwezi kuponya majeraha ya wanawake wetu,kuwapenda na kuwapa nafasi kwenye maamuzi na umiliki Mali Kati yetu,hatuwezi kufika mbinguni Kama wanawake wetu wataendelea kuishi chini ya vivuli Vya maamuzi kandamizi na yenye kununua roho ya kiungwana na kuamini kwenye Uhuru wa maoni yao wenyewe ambazo ni hekima ndani yao.
Duniani Hakuna Amani maana Kuna Vita ya kisaikolojia Kati ya mwanamke na mwanaume,tumetengwa mbali Sana kutokana na maandiko hayo matakatifu,maandiko hayo yanamuhukumu mwanamke Sana na kumfanya kiumbe kibaya duniani,maandiko hayo yanawafanya wanaume kuwaona wake zao kuwa ni wasaliti tayari,wanaishi kwa kuviziana n'a kufichana Mambo,mke n'a mume wanaishi Basi tu ila Wana vita ndani yao,watu hawaaminiani sio kwa kuwa ni Tabia Basi tu kwa kuwa fulani waliandika tayari....
DUNIA ITAKUWA SEHEMU SALAMA KAMA WANAUME WAKIAMUA KUFIKIRI BILA BOKSI,WAKIAMUA KUTENGENEZA NJIA YENYE USAWA NA SALAMA KWA WOTE DUNUANI,WANAWAKE WETU WANA HASIRA NA SISI KWA KUWA TUMESHINDWA KUTATUA MATATIZO NA KAZI YA MWANAUME NI KUTATUA MATATIZO,HUU NDIO UKWELI

Maoni