Furaha Ni Nini?
Watu wengi hudhani furaha Ni kufanya starehe nyingi au mbalimbali au kuwa na vitu vingi vinavyokupa starehe. Wengine hudhani furaha Ni kuwa na watu Fulani karibu Yako kila Mara,huenda ikawa Ni kweli kwa baadhi ya watu panda wakati mwingine hukufanya ujisikie nafuu kutokana na madhila ya maisha.... Wengine huenda Mbali zaidi na kuwategemea watu kuwa Ni sehemu ya kujipatia furaha... Bila kujua matarajio ya binadamu mwenzio kukupa furaha Ni madogo Sana. Je furaha Ni Nini Basi!? Furaha Ni amani thabiti kutoka ndani ya moyo wa mtu,ni amani inayoambatana na imani ya kweli na yenye uchanya ndani yake,kuwa na furaha sio kukosekana kwa matatizo au tabu mbalimbali hapana ni kukubaliana na hali fulani ya wakati uliopo huku ukipambana kuibadilisha au kuimarisha iwe salama na bora zaidi. Furaha ni usalama wa hisia zako unaochangiwa na msukumo wa ndani yako mwenyewe wala hapana yeyote anaweza kutoka nje yako na kuijaza furaha ndani yako, ni lazima uwe mtu mweny...