Isabella-sehemu ya 01

        Wakati mwingine moyo unaweza ukafanya macho yakawa mapofu na yasione uendapo,wakati mwingine pia macho huweza kuudanganya na kuhadaa moyo usiweza kuchagua na kujua kipi bora na kipi sio bora chakuacha,ni kweli kuwa macho huona na moyo hutamani,pasipo matamanio hakuna kupenda wala kuvutiwa na chochote,akili nazo hujiona ni bora na kuwa na matakwa makubwa kuliko chaguzi LA moyo,fikra ni vitu bila fikra hakuna kitu chochote.
        Isabella ni msichana mrembo mwenye umri mdogo ambaye amelelewa katika mazingira au makuzi ya kimaadili na mapenzi makubwa kutoka kwa wazazi,ubora wa familia alotokea haukuwa unafanana na  na hata mmoja wa marafiki ambao amewahi kuwa nao wala ambao amewahi kusoma nao.Alikuwa anaishi kwenye jumba ambalo hakukusa chochote wala hakuwa na shida yoyote.Alisoma tangu elimu ya awali mpaka elimu ya juu kwenye shule za kisasa na za gharama kubwa huku baba yake akiwa mfanyabiashara wa madini na mama akiwa ni daktari.
     Isabella alikuwa na wadogo zake wawili ambao nao waliishi maisha ya kifahari na wasijue kinachoendelea nje ya kuta za jumba lao na matatizo makubwa au shida ambazo watu wengine wamewahi kuwa nazo au ambazo watu Fulani hupitia,waliishi wakifurahi na wala hakuna ambacho wamewahi kukikosa.Amani ndio alimfuata Isabella na wa mwisho aliita Lucy.
     Kutokana na shughuli za kiuchumi za familia yao baba alikuwa ni mtu wa kusafiri kibiashara na mama alikuwa ni daktari bingwa wa upasuaji ambaye alitegemewa sana na hospitality mbali mbali nchini hivyo ilikuwa akisafiri Mara kwa Mara kutoa huduma sehemu mbali mbali,hata na hivyo haikuwa sababu ya kuacha kuwapenda na kuwapa watoto wao mapenzi na Upendo na mafunzo yaliyo bora,walikuwa wakirudi Mara kwa Mara kuwapa moyo watoto na kuwafariji,kuwalea vyema na kuwatimizia mahitaji yao kama ilivyo kwa wazazi ni jukumu lao.
     Siku moja wakiwa nyumbani familia wote,walikula pamoja na kufurahi sana ilipofika wakati wa kulala mama aliwaandalia wanawe sehemu salama pakulala huku isabella na baba yake wakiwa bado wanazungumza maendeleo yake ya kitaaluma,ghafla kilisikika kishindo nje ya mlango wao na mlio mkubwa wa bunduki ambao uliharibu kabisa kitas cha mlango,walitokea watu wasojulikana na kumteka Isabella wakimtaka baba yake awape fedha LA sivyo watamuua,mzee alitii Amri na kuwapa fedha hizo,hata hivyo haikuwa mwisho walimuua baba isabella mbele ya isabella na kumbaka mama isabella mbele ya watoto wake.
     Kutokana na uchungu wa mama aloupata wa kitendo cha kufanyiwa uchafu mbele ya wanawe alishindwa kujizuia na kunywa vidonge ambavyo vilipelekea kuupoteza uhai wake huku akiiacha familia katika wakati mgumu na wa majonzi makuu wakiwa hawana msaada wala hawajui pakuanzi.

Itaendelea................

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Bin bin pyramid

Japan vs costa rica

MANUEL DE LA SUPRÉMATIE BLANCHE