Isabella-sehemu ya 02
Baada ya msiba mkubwa ulioufika familia ya isabella,ndugu na jamaa na marafiki walifika kufanya taratibu mbali mbali za maziko ambapo watu wengi walijawa na simanzi na nyuso za huzuni kutokana na msiba mkubwa ambao watoto hao wamefikwa,taratibu mbalimbali zilifanyika na siku inayofuata maziko yalifanyika kuwahifadhi wapenzi hao wawili kwenye nyumba yao ya milele.
Isabella na wadogo zake walikuwa wenye uchungu mkubwa haswa ikitegemewa kuwa wao bado ni tegemezi na ni watoto bado,isabella alikuwa kidato cha pili katika shule moja hapa jijini huku wadogo zake wakiwa bado katika shule za msingi,Baada ya msiba ndugu walikaa kikao ambacho kilikuwa kikiamua nani awe msimamizi na kuwakuza watoto na Mali mbali mbali za wazazi wao ikiwa ni pamoja na migodi ya madini iliyopo mererani,ilifikiwa muafaka kwamba Dada yake na marehemu shangazi yao ndio atakayesimamia na kuendeleza biashara mbalimbali za marehemu huku akiwalea watoto wake.
Ndugu na Jamaa walitawanyika baada ya msiba Kumalizika na kuwaacha watoto na shangazi yao huku wakiwa na tumaini kuwa shangazi ni mtu wa karibu na marehemu na atawatunza watoto vyema,huo ndo ukawa mwanzo wa maisha mapya ya isabella na nduguze wawili ambao walikuzwa kwenye makuzi ya upendo mkubwa na kudeka kwa wazazi wao.Shangazi alihamia kwa kin isabella na kuanza kuishi hapo na alikuwa mwema sana kipibdi cha mwanzo na kujitahidi kuonyesha Upendo na kuwafariji watoto kwani walikuwa katika wakati mgumu wa kuanza kuyazoea mazingira mapya bila ya baba wala mama.
Isabella akarudi shuleni alipokuwa anasomea kwani while zilifunguliwa huku akiwaacha wadogo zake nyumbani na shangazi take kwani aliamini kuwa wapo katika sehemu salama na watalelewa vyema,alifika shuleni na kuitwa ofisini kwa mwalimu mkuu wa shule ambaye alianza kumpa ushauri na kumtia moyo kwani alijua yupo kwenye kipindi kigumu kwenye maisha yake,alirudi na kuingia darasani hats hivyo alikuwa bado ni mnyonge mwenye mawazo mengi na wakati mwingi alikuwa akilia.Mwalimu aliamua kumtoa nje kwani alijua kabisa hakuna anachoelwa licha ya kwamba alikuwa ni mmoja kati ya wanafunzi bora darasani na mwenye bidii kubwa.
Marafiki zake walijitahidi sana kumliwaza na kumtia moyo kwani walimpenda sana na licha ya kwamba alitoka kwenye familia za halo ya juu ya sliver spoon family hakuwa akijionesha wala kujikweza kwani alikuwa ni binti mwenye Upendo na mwenye moyo wa kuwasaidi wengine,hakika isabella ni Binti mrembo na alionekana licha ya kuwa na umri mdogo alivutia sana na kila Mara marafiki zake walikuwa wakimsifia na kumueleza jinsi alivyojaaliwa na muumba.Baada ya muda kupita alionekana furaha yake ikianza kurejea na kujichanganya na wanafunzi wenzake na kujisomea huku akiendelea na kujituma kwani alijua elimu ndio mkombozi wake aliyebaki.
Itaendelea

Maoni