Isabella-sehemu ya 04

    Sauti ya nguvu na ukali ilisikika ikitoka ndani na Mtoto akilia kwa uchungu huku akimuita mama upo wpi,huku sauti ya Mtoto ikisikika akilia ghafla geti lilifunguliwa kwa Sauti ya kubamiza na ghafla akaonekana Mtoto mdogo wakike akirushwa nje ya geti huku wakiume akjmfuatia na kumnyanyua Dada yake na kumodolea macho alowatoa nje ya geti,huku akiwahimiza wapotee mbele ya macho yake waende shuleni,watoto wawili wadogo kabisa hao wakiwa hawajui lakufanya nilisikia sauti ya yule wakiume akisema shangazi bus LA shule halipo.
    Kumbe ni Lucy na Alex ndo walikuwa wakinyanyaswa na shangazi yao huyo aloachiwa kuwalea pamoja na kusimamia Mali mbalimbali za baba yao.ilisikika sauti ikisema
(Bus lashule halijaja kwani baba yako yupo hapa awalipie hela ya bus LA kuwapeleka shuleni?) Oh kumbe ni shangazi ndo alikuwa akiwajibu watoto aloachiwa kuwalea na kuwatunzia Mali za baba yao ili wakikua wakaidhi.watoto wale walianza kuondoka taratibu kwa unyonge Alex akiwa amemshika Lucy mkono huku watu waliowaona watoto hao wakiulizana kulikoni? Lucy alikuwa akilia njia nzima hulu Alex akimtuliza na kumsihi anyamaze hata hivyo haikuwa rahisi kwani no ghafla sana kukutana na mazingira waliopo kwa sasa.na ukizingatia mtaa wanaoishi watoto wote walikuwa wakipelekwa na school bus ila wao walitembea kwa miguu tangu siku  hiyo.
    Ghafla gari aina ya brado iliwapita kwa kasi kubwa na kuwapulizia vumbi huku lucy akisema gari ya baba ilee,kumbe ni shangazi yao aliwapita kwa kasi hiyo akijifanya anawahi kwenye shughuli zake za kibiashara mapema ile,maskini weeee watoto wote walilia kwa uchungu kwani walizoea kuwa baba yao huwa alikuwa na mazoea ya kuwapeleka shuleni kwa gari anapokuwa yupo nyumbani na kutokana na mazoea hayo iliwauma sana kuona kuwa Mali zao zinawanyanyasa na kuwatia simanzi kubwa.walipokuwa hapo wakilia alipita jirani na rafiki tu wa baba yao na kuwakuta na kuwauliza kulikoni na kwanini wanalia,Alex alisema RU kuwa gari LA shuleni liliwaacha,basi bila hiyana aliwapeleka hadi shuleni na kuwakabidhi kwa mwalimu wao wa darasa.
  Kwanini haujafua nguo?? Na kwanini chooni pachafu? Sauti hiyo Kali ilisikika kutoka ndani na wtoto walianza kulia sana,kumbe watoto wale walianza kujifulia wenyewe na hata wakati meingine usafi walikuwa wakifanya,shangazi hakuwa kabisa na huruma wala msaada kwa watoto Bali alikuwa ni chanzo cha huzunj,manyanyaso na mateso kwa watoto wale,toka kafue nguo halafu wewe Fanya usafi chooni haraka nikifunga macho nikifungua nikute vyote visafi,halafu Alex ukimaliza kufua ukaoshe vyombo vyote umenielewa!? Alex alijibu kwa kutingisha kichwa tu kwani alimuogopa sana shangazi kwani wakati mwingine alikuwa akiwapiga,na wakati mwinhine kuwalaza njaa.
  Walipomaliza shughuli zao,walikuwa tu wakijichezea barazani kwao mchezo wa kukimbuzana huku shangazi akiwa ndani na marafiki zake wakizogoa,alex aliamua kuingia kuwasha TV kuangalia vipindi vya watoto.Shangazi alimwambia atoke nje na asirudi mpaka amwite na endapo atakaidi hatokula siku hiyo,alitoka na mpaka giza limeingia alijikalia barazani na hata baada ya hapo hakuitwa mpaka usiku wa saa  nne  ndipo shangazi alimwambia aingie ndani na aoge alae alale .
Itaendelea.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Bin bin pyramid

Japan vs costa rica

MANUEL DE LA SUPRÉMATIE BLANCHE