Njia 3 za kujua kuwa upo kwenye mahusiano yasiyo sahihi

   Wote tupo tunajua kuwa maisha yetu ni muungano wa watu wawili,wrot huwa tunatarajia kuona maisha yeru yakiwa yenye furaha na upendo na amani ndani yetu.
   Tunapaswa kutambua kuwa maisha ya upendo ni lazma ila maisha ya mahusiano ni uchaguzi,ni chaguo la mtu kuwa nawe kwenye mahusiano na sio lazima mtu kuwa nawe kwenye mahusiano.watu Fulani huwaganda watu wakidhani kuwa ni hali yao na ni lazima wawe nao kwenye mahusiano kumbe mahusiano ni mtu akuchague,sio lazima mtu akikupenda awe nawe kwenye mahusiano ila ni lazima mtu akikuchagua kuwa nawe kwenye mahusiano akupende.
  Jinsi ya kujua kuwa upo kwenye mahusiano bandia.

1:USIRI;Watu wengi ambao wapo na watu wasio sahihi kwanza sio wawazi,hawawaweki waliopo nao kwenye mahusiano wazi kwa watu wao wa karibu,huwa wanapenda kuwa na usiri huku wakijitetea muda bado au tusubiri tuwe tayari.Hakika nakuambia kuwa hakunaga muda sahihi wa mtu kuwa kwenye mahusiano au ndoa ni maamuzi tu watu wengi hudhani kuwa muda ndio huwafanya kuwa kwenye mahusiano ila sivyo ni maamuzi tu,kama anakuficha basi jua sio sahihi.
2:UONGO;Kwa mtu akupendaye kwa dhati daima atakua mkweli na muelewa,atakueleza yaliyo sahihi,haijalishi kakosea kiasi gani husema kweli na kutaka radhi.Watu wengi waongo ni huwa hawapo kwenye mahusiano wa aina moja huwa wapo na wapenzi wengi na hivyo ndivyo uongo huwa,tambua uongo huhitaji uongo mwingine ili kuwa uongo kamili,kama unadanganywa basi jua hapo umelamba tasa.
3:MAIGIZO;Mtu asokupenda na anayekuchukulia poa anakua na maigizo mengi anapokutana na wewe.Wakati mwingine anaweza kuigiza hata mbele ya walio karibu yako au ya walio karibu yake ili kuficha kuwa tupo nawe,hapa sio sahihi chunga sana.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Bin bin pyramid

Japan vs costa rica

MANUEL DE LA SUPRÉMATIE BLANCHE